We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Friday, June 21, 2019

Ukiona mtu anazunguka kuichafua nchi yake huyo hayuko sawa - Dkt.Abbassi


Wanadiplomasia na wanataaluma ya mawasiliano nchini, wametakiwa kuitangaza Tanzania katika mahusiano ya kitaifa na kimataifa kwenye masuala ya amani,utulivu wa kisiasa na sera nzuri ili kuwavutia watalii na wawekezaji kuja nchini, hatua ambayo itakuza pato la Taifa.

Hayo yamebainishwa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, wakati akizungumza na wanachuo wa mwaka wa pili wa Shahada ya Mawasiliano ya Umma wa Chuo cha Diplomasia, Jijini Dar es Salaam kwenye mjadala maalum kuhusu Mahusiano ya Umma na ya Kimataifa.

Dkt Abbasi alisema ni muhimu kwa wanataaluma wazalendo kuitangaza nchi yao kwa mazuri ili fursa pana za uwekezaji zilizopo kuwafikia wawekezaji na watalii kuitumia nafasi hiyo ambayo pamoja na kujenga mahusiano mazuri baina ya Tanzania na nchi mbalimbali pia itaongeza imani kubwa kwa jamii za kimataifa.

“Ni muhimu kwa wanadiplomasia na Wanamawasiliano wetu wa Kitanzania tukaitangaza nchi yetu, Tanzania ni nchi ya amani,hata kama kuna wanaojaribu kuitangaza vibaya nchi yetu wataumbuka tu iwapo sisi wanataaluma tutasimama kidete kuitetea”,alisema Dkt Abbasi.

Kila Mtanzania ana wajibu wa kuiongelea vizuri Nchi yake, ukiona mtu anazunguka huko Duniani kuichafua nchi yake huyo hayuko sawa”,alimalizia Dkt Abbasi.

Dkt.Abbasi pia alizungumzia ukuaji wa uwekezaji nchini, ambapo alisema katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli zaidi ya viwanda 3,000 vimefunguliwa na hivyo kuongeza pato la Taifa na ajira kwa watanzania.

Aidha aliwataka wanataaluma ya mawasiliano kwa umma kuwa kiunganishi kati ya taasisi na jamii katika kuzungumzia masuala ya kimaendeleo na akasisitiza kuepuka propaganda.

Dkt. Abbasi pia alisema katika ukanda wa Afrika Mashariki kwa sasa Tanzania inaongoza kuwa na wawekezaji wengi hatua ambayo imetokana na kuwepo na sera nzuri za biashara na uwekezaji.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list