Kiungo Haruna Niyonzima amethibitisha kuwa hatakuwa sehemu ya kikosi cha Simba kwa ajili ya msimu ujao
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Niyonzima amewashukuru mashabiki wa Simba kwa ushirikiano waliompa wakati wote
Aidha amesema wakati ukifika ataweka hadharani klabu atakayojiunga nayo
"Nashukuru kwa kumbukumbu nzuri tuliyotengeneza tukiwa sote. Wakati ukifika nitaweka hadharani ninapoelekea..," ameandika Niyonzima
Mnyarwanda huyo ni miongoni mwa wachezaji ambao hawakupendekezwa kuongezewa mikataba na kocha Patrick Aussems

No comments:
Post a Comment