Maelfu ya raia nchini DR Congo wameendelea kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa kinara wa upinzani na wakati mmoja waziri mkuu wa nchi hiyo, Etienne Tshisekedi.
Mwili wa Tshisekedi uliwasili nchini DRC Alhamisi ya wiki hii ukitokea nchini Ubelgiji ambako ulikuwa umehifadhiwa kwa zaidi ya miaka miwili.
Jumla ya viongozi sita wa Afrika wanatarajiwa kuhudhuria mazishi yake akiwemo rais wa Angola, rais wa Rwanda Paul Kagame, rais wa Togo na nchi jirani ya Congo Brazzaville.
Tshisekedi alifariki akiwa mjini Brussels February 2017 akiwa na umri wa miaka 84, ambapo ameshindwa akushuhudia kuapishwa kwa mwanawe Felix Tshisekedi ambaye amekuwa rais wa DR Congo kupitia uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
Mwili wa Tshisekedi umewekwa katika uwanja wa mpira wa Stade Martyr ambapo wananchi wanapata nafasi ya kutoa heshima za mwisho kabla ya mazishi yake siku ya leo kwenye mji wa Nsele nje kidogo ya jiji la Kinshasa.
No comments:
Post a Comment