Kipute cha michuano ya kombe la Azam (ASFC) maarufu kama kombe la FA, kinafika tamati leo kwa mchezo wa fainali kati ya Azam Fc dhidi ya Lipuli utakaopigwa uwanja wa Ilulu mkoani Lindi
Lipuli Fc iliiondoa Yanga kwenye hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa mabao 2-0 wakati Azam Fc ilifika hatua hiyo kwa kuifunga KMC bao 1-0 kwenye mchezo wa nusu fainali
Mshindi wa mchezo huo unaotarajiwa kuanza saa tisa Alasiri atapata kombe na fedha Taslim Tsh Milioni 50
Pia atapata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania Bara kwenye michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu ujao
No comments:
Post a Comment