Leo klabu ya Simba imetangaza nafasi za kazi ambapo miongoni mwa nafasi hizo zilizotangazwa ni nafasi ya Afisa wa Habari
Wengi wamekuwa wakijiuliza kuhusu hatma ya Haji Manara ambaye amekuwa Afisa Habari wa Simba kwa zaidi ya miaka minne
Manara amewatoa hofu mashabiki wa Simba akiwahakikishia kuwa ataendelea kuwepo Msimbazi
Aidha Manara amepongeza utaratibu wa Simba kutangaza nafasi za kazi kwani utaiwezesha timu hiyo kupata watu sahihi wa kusimamia majukumu ya kiutendaji ya kila siku
"Huu ni utaratibu sahihi na ndio hufuatwa na taasisi nyingi zilizobadisha muundo," ameandika Manara kwenye ukurasa wa Instagram
"Ndio, Simba kwa sasa ni Simba SC Limited, hivyo kutangaza upya nafasi za ajira kwa wafanyakazi ni jambo sahihi kabisa"
"Mnaohoji uwepo wangu klabuni, nipo sana kwa Inshallah,ondoeni hofu na wale wanaodhani kutakuwa na ahueni labda wakidhani sipo, hapana nipo na mtaambiwa kwa nafasi gani"
No comments:
Post a Comment