Mapema leo Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla alisema kuwa timu hiyo imefanikiwa kuwasajili wachezaji wote wa ndani na nje waliopendekezwa na kocha Mwinyi Zahera
Hata hivyo mabosi wa Kamati ya usajili chini ya Mwenyekiti Frank Kamugisha, walilazimika kusafiri hadi nchini Misri kukamilisha usajili wa baadhi ya nyota ambao wanashiriki fainali za Afcon 2019
Farouq Shikalo ni mlinda lango aliyekuwa akisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Yanga
Usajili wake ulizungumzwa tangu mwishoni mwa mwaka jana baada ya Kamati ya usajili wakati huo ikiwa chini ya Hussein Nyika kushindwa kumnasa wakati wa usajili wa dirisha dogo
Shikalo amesaini mkataba wa kuitumikia Yanga akiwa nchini Misri pamoja na beki Ali Mtoni 'Sonso' anayetua Yanga akitokea klabu ya Lipuli Fc
No comments:
Post a Comment