We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Friday, June 28, 2019

Licha ya Taifa Stars kufungwa na Kenya, Waziri Kigwangalla awapongeza na kuwaahidi zawadi nono ‘Mmetufikisha juu sana’

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameipongeza timu ya Taifa Stars kwa kuitangaza nchi kimataifa licha ya matokeo kuwa sio mazuri kwenye michuano ya AFCON inayoendelea nchini Misri.

Image result for kigwangalla Taifa stars
Waziri Kigwangalla

Waziri Kigwangalla ametoa pongezi hizo kupitia ukurasa wake wa Twitter kwa kusema kuwa “Watu wangu wa nguvu, msiumie, msisononeke. Mmetupa heshima, mmetufikisha juu sana. Matokeo ni kitu kingine, mmeitangaza nchi yetu parefu sana. Safari na iendelee.”.
Kwa upande mwingine, Waziri Kigwangalla amewapa ofa wachezaji wote wa Taifa Stars kutembelea hifadhi za taifa kwa ajili ya mapumziko pindi watakaporudi nchini.
Kumbukeni mna offer yangu ya kwenda kupumzika kwenye hifadhi zetu. Kazi kwenu kuitumia” ameandika Waziri Kigwangalla.
Jana Taifa Stars ilipoteza mchezo wake wa pili wa AFCON 2019 dhidi ya Harambee Stars ya Kenya. Matokeo ambayo yameifanya Tanzania kutolewa kwenye michuano hiyo licha ya kubakiza mchezo mmoja dhidi ya Algeria.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list