Kiungo Francis Kahata anatarajiwa kuchukua nafasi ya Haruna Niyonzima ambaye uongozi wa Simba umamua kutomuongezea mkataba
Inaelezwa usajili wa Kahata tayari umekamilishwa nchini Misri na mabosi wa Simba ambao juzi walikuwepo wakati Harambee Stars ikimenyana na Tanzania
Simba ilianza kumfuatilia Kahata kabla ya kuanza michuano ya Afcon, hata hivyo kiungo huyo aliyemaliza mkataba Gor Mahia aliomba amalizane na mabingwa hao wa Tanzania Bara baada ya michuano ya Afcon kumalizika
Hata hivyo Simba inahitaji kumtumia kwenye michuano ya ligi ya mabingwa ambao usajili wake unapaswa uwe umekamilika kesho
Hivyo kuwalazimu mabosi wa Simba kumfuata hukohuko Misri kumalizana nae
Mabosi hao pia wako Misri kumaliza na mshambuliaji Emmanuel Okwi ambaye mpaka sasa ameifungia Uganda mabao mawili michuano ya Afcon
No comments:
Post a Comment