Mlinda lango Deogratius Munishi 'Dida' amemaliza mkataba kunako klabu ya Simba na amewaaga mashabiki wa timu hiyo kwa ushirikiano aliopata mwaka mmoja alioitumikia Simba
Munishi amesema kwa sasa yeye ni mchezaji huru baada ya mkataba wake na Simba kumalizika
Amesema katika umri wa miaka 30, anahitaji changamoto nyingine
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Dida ameandika;
"Namshukuru Mungu nimemaliza salama msimu wa 2018/19 na nimemaliza salama mkataba na Simba S.C"
"Nawashukuru watu wote tulioshirikiana katika msimu mzima ulikuwa na mafanikio chanya kwa Club"
"Katika umri wa miaka 30 nikiwa MCHEZAJI HURU nahitaji kupata changamoto mpya mahala pengine"
No comments:
Post a Comment