We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Sunday, June 30, 2019

AZAM TV - HABARI 30.06.2019

Bonyeza play hapa chini kutazama zaidi pia tembelea app hii kila Mara kusoma habari mpya

TAMTHILIYA: MANENO YA KUAMBIWA EP - 50


Bonyeza play hapa chini kutazama zaidi pia tembelea app hii kila Mara kusoma habari mpya

Waziri aagiza wakandarasi kuendelea kushikiliwa


Waziri wa Nishati Medard Kalemani ameuagiza uongozi wa mkoa wa Shinyanga kuendelea kuwashikilia wakandarasi wa kampuni ya Angelique International LTD inayosambaza umeme wa REA katika maeneo ya Shinyanga vijijini na maeneo ya wachimbaji wadogo ya Mwakitiliyo hadi watakapomaliza kusambaza na kuwasha umeme katika vijiji vyote na kukaguliwa. 

Waziri Kalemani ametoa kauli hiyo wakati akikagua utekelezaji wa maagizo aliyotoa akiwa katika ziara mkoani Shianyanga mwanzoni mwa mwezi huu na kubaini utendaji usioridhisha wa wakandarasi hao ambapo amedai kuwa kwa sasa ameridhika kidogo 

Nao baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mwakitolyo ambacho kilirukwa na umeme wa REA wameipongeza serikali kwa kusikiliza malalamiko yao na kuyafanyia kazi kwa haraka na kwa kipindi cha wiki mbili wameshapata umeme kwa maelekezo ya waziri huku kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bi. Nyabaganga Daudi Taraba ambaye pia ni kuu wa wilaya ya Kishapu akimueleza waziri kalemani kuwa bado kasi ya kuunganisha umeme katika maeneo yaliyofikiwa ni ndogo kutokana na mwamko mdogo wa wananchi kulipia. 

Katika hatua nyingine Waziri Medard Kalemani amemuagiza meneja wa Tenesco mkoa wa Shinyanga kusimamia ujenzi wa njia za umeme katika eneo la mwakitilyo ziunganishwe vizuri ili Mwakitolyo iwe kijiji cha mfano huku meneja wa Tanesco Shinyanga Fedigrace Shuma akidai kuwa changamoto kubwa inayofanya zoezi liende taratinu ni uchimbaji wa mashimo ya kusimika nguzo kutokana na eneo kuwa na mwamba mgumu.

Ulimwengu akanusha kutua Yanga


Mshambuliaji wa JS Saoura ya Algeria, Thomas Ulimwengu amekanusha taarifa za kuhusishwa kujiunga na Yanga.

Ulimwengu na Mbwana Samatta wanashikilia rekodi ya kuwa wachezaji wa Tanzania kuchukua kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika (2015) wakiwa na kikosi cha TP Mazembe.
Hata hivyo aliamua kuondoka katika kikosi hiko baada ya mkataba wake kumalizika ndipo tetesi za kujiunga na klabu za nyumbani Simba na Yanga zilianza, lakini baadae akaibukia katika kikosi cha Al Hilal, Sudan.
Akiwa katika kikosi hiko hakudumu sana na alienda kusajiliwa katika kikosi cha Js Saoura ambacho anakitumikia mpaka hivi sasa.
Hivi karibuni ziliobuka tetesi za mshambuliaji huyu kuhitajika na Yanga, lakini ameamua kutolea uvivu jambo hilo kupitia katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii.
"Nimesikia tetesi nikihusishwa kusaini na timu moja ya Tanzania, hizo taarifa siyo za kweli," aliandika Ulimwengu.

Watoroshaji dhahabu katavi kukiona


Mkuu wa mkoa wa Katavi  Juma Homera aapa kupambana na wanaotorosha dhahabu huku mpaka sasa watu wawili wakishikiliwa na jeshi la polisi kwa kununua dhahabu kinyume cha sheria mkoani humo.

RC Homera akiwa ziarani katika migodi mbalimbali ikiwemo dilifu ambao ni mgodi wa wachimbaji wadogo na mgodi mkubwa wa Katavi na Kapufi mining  alieleza anachotaka wachimbaji wadogo wakauuze madini yao katika soko la madini la mkoa huo.

Homera alianza majukumu ya ukuu wa mkoa ikiwa soko limeshafanya biashara kwa kununua dhahabu gram 238, May 23/2019 jambo ambalo lilimfanya aanze kufatilia na kubaini dhahabu nyingi inayopatikana Mkoani Katavi inauzwa nje ya mkoa wa  Katavi nakupelekea soko hilo kusua sua.

Kufuatia jambo hilo limemfanya  Homera kuyafanyia kazi mapungufu ya soko hilo, mpaka sasa ununuzi na uuzaji wa madini ni Grams 6317.2 sawa na Kg 6 na Grams 317.2 yenye thamani ya Tshs.Million 519,155,127.56 zimenunuliwa kwa kipindi cha Mei na June 30/2019 na serikali kupata mrahaba (Royality7%) Tsh Milioni 36,340,858.92 na Service levy  0.3% Tsh.milioni 1,401,718.85.

Aidha ameimarisha mifumo ya Benk mbili katika soko hilo na ameendelea kuwabana mablokers na wanunuzi wenye leseni na wachimbaji mbalimbali  kuhakikisha pia wanauza madini yao kwenye soko la mkoa ili tujenge uchumi wa Tanzania na kumuunga mkono Rais wetu Dkt.John Joseph Pombe Magufuli katika kuinua uchumi na miundombinu ya nchi hii kwa kulipa kodi.

Mkataba wa udhamini Simba, Mo Xtra kusainiwa Jumatatu

Klabu ya Simba kwa kushirikiana na kampuni ya A-one wazalishaji wa kinywaji cha Mo Xtra, kesho Jumatatu watasaini mkataba wa udhamini

Walichozungumza abiria wa ATCL safari ya kwanza ya ndege hiyo Afrika Kusini

Abiria wanaotumia usafiri wa Kampuni ya ndege yaTanzania ATCL kutoka Dar es salaam kwenda Afrika Kusini wamevutiwa na huduma ya usafiri zinazotolewa na kampuni hiyo huku wakiomba kuwekeza ndege nyingi zaidi kutokana na kasi ya watumiaji kuongezeka.

Bonyeza play hapa chini kutazama zaidi pia tembelea app hii kila Mara kusoma habari mpya

Pembe za Faru zinaongeza nguvu za kiume? Sikiliza ukweli hapa...

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Hamis Kigwangalla amewataka watu kuachana dhana potofu kuwa pembe za faru zinasaidia kuongeza nguvu za kiume na kuongeza kuwa huo ni uzushi na pembe hizo hazina msaada wowote katika kuondoa tatizo hilo.

Bonyeza play hapa chini kutazama zaidi pia tembelea app hii kila Mara kusoma habari mpya

LIVE: TAZAMA TAARIFA YA HABARI YA TBC ONE

Bonyeza play hapa chini kutazama zaidi pia tembelea app hii kila Mara kusoma habari mpya

LIVE: TAZAMA TAARIFA YA HABARI YA ITV

Bonyeza play hapa chini kutazama zaidi pia tembelea app hii kila Mara kusoma habari mpya

LIVE: TAZAMA TAARIFA YA HABARI YA CHANNEL TEN

Bonyeza play hapa chini kutazama zaidi pia tembelea app hii kila Mara kusoma habari mpya

TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO JUMAPILI

Arsenal italazimika kuilipa Crystal Palace pauni milioni 100 kumnasa mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfred Zaha, 26. (Mail on Sunday)
Lakini mwenyekiti wa Eagles, Steve Parish anahofu kuwa kumuuza Zaha kunaweza kuhatarisha mipango yake ya kuwapata wamiliki wapya. (Sun)
Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Jacob Bruun Larsen amezivutia timu za Liverpool, Manchester United na Arsenal.(Mail)
Mwenyekiti wa klabu ya Tottenham Daniel Levy amewapigia simu Rea Madrid akitoa ofa ya mchezaji Christian Eriksen, ambaye amekataa kuongeza mkataba wake na Spurs baada ya majira ya joto mwaka 2020. (Marca)

Christian EriksenHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 20, amebakiwa na miaka mitatu katika mkataba wake na Paris St-Germain na hana mpango wa kuongeza mkataba kuendelea kuichezea klabu hiyo. (Marca)
Makamu mwenyekiti wa Manchester United Ed Woodward amewaambia wafanyakazi wake kwa kuwa klabu ina mipango ya kuongeza wachezaji ''vigongo'' msimu huu baada ya kumaliza mchakato wa kumnaa Aaron Wan-Bissaka. (Sunday Telegraph)

Alvaro MorataHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Paul Pogba atafanya mazungumzo na Kocha Ole Gunnar Solskjae juma lijalo, kuhusu mipango ya kuondoka Old Trafford. (Sun)
Mshambuliaji wa Birmingham City na timu ya taifa ya England Che Adams ameagana na wachezaji wenzake kabla ya kuhamia Southampton. (Mail on Sunday)
Southampton wamekubali kumuuza beki wa kushoto Matt Targett kwa Aston Villa kwa kitita cha pauni milioni 14. (Sunday Telegraph)
Liverpool na Tottenham wamejiweka mbali na mchakato wa kumchukua Bruno Fernandes, na kumfanya kiungo wa kati wa Sporting Lisbon kujiunga na Manchester Unted. (Sunday Express)
Kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino amesema hana kauli ya mwisho kuhusu malengo ya uhamisho.
Spurs wanategemea kumaliza mchakato wa kumnasa kiungo wa kati wa Lyon Tanguy Ndombele, 22 kwa kitita cha pauni milioni 60. (Standard)

NdombeleHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Chelsea wameitahadharisha Atletico Madrid kuwa watasitisha mkopo wa mshambuliaji Alvaro Morata, iwapo Atletico Madrid hawatatoa pauni milioni 50 kwa ajili ya uhamisho wa kudumu. (Sunday Telegraph)
Inter Milan inahitaji kukusanya kiasi cha pauni milioni 75 kumnasa mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 26, kutoka Manchester United, fedha zitakazopatikana baada ya kuumuza kiungo wa kati Joao Mario, 26 na beki wa kushoto Dalbert, 25. (Sun on Sunday)
Mabingwa wa Italia Juventus wameingia makubaliano na Paris St-Germain kumnasa kiungo wa kati Adrien Rabiot. (Sky Italy, Sky Sports)
Mlinda mlango wa Cameroon na Ajax Andre Onana anasema anataka kubaki na timu hiyo ya Uholanzi ingawa Manchester United imekuwa ikionyesha nia kwa mchezaji huyo. (Voetbal International, via Metro)
Watford wamefikia makubaliano kumsajili mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa timu ya West Brom Craig Dawson kwa kiasi cha pauni milioni 5.5. (Sky Sports)
Millwall na Bristol City watapambana kumnyakua mshambuliaji wa Barnsley Kieffer More.(Mail on Sunday)
Leeds United wanakaribia kumnasa winga wa Wolves, Helder Costa 25.(Birmingham Mail)

Hivi ndivyo Okwi anavyoisumbua Simba

Mshambuliaji wa Simba na timu ya taifa ya Uganda, Emmanuel Okwi ameendelea kuuwasha moto katika michuano ya mataifa ya Afrika inayoendelea nchini Misri.

Okwi ambaye alimaliza msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita kwa mabao 16, amekuwa msaada mkubwa katika kikosi cha Uganda 'Cranes' ambacho kimefanikiwa kushinda mechi moja na kutoa sare moja katika michuano ya AFCON, huku mwenyewe akifunga mabao 2 mpaka sasa.
Hali hiyo imezidi kuwatamanisha mabosi wa Simba ambao wanamuhitaji mchezaji huyo katika msimu ujao wa ligi, ambapo mpaka sasa wanahangaika kupata saini yake, huku mkataba wake ukiwa ukingoni kumalizika ndani ya Msimbazi.
Inaelezwa kuwa tayari mabosi wa Simba wametua nchini Misri ili kumalizana na mchezaji huyo, ambapo mwenyewe amekuwa akisita kuweka wazi endapo ataendelea kubakia Msimbazi msimu ujao au ataondoka, akisisitiza kuwa hawezi kusema chochote hivi sasa michuano ikiwa inaendelea.
Simba imewasainisha mikataba mipya wachezaji wengi waliokuwa nao msimu uliopita wakiwemo, Aishi Manula, Erasto Nyoni, Meddie Kagere, Shomari Kapombe, John Bocco, Mohamed Hussein na Jonas Mkude, huku kikwazo kikubwa kikiwa ni kwa Okwi ambaye bado hajaridhia kumwaga wino katika klabu hiyo.
Usiku wa leo majira ya saa 5:00, Uganda itaingia dimbani kuvaana na wenyeji Misri katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya michuano hiyo. Endapo Uganda itapata ushindi au sare yoyote katika mchezo huo itakuwa imejihakikishia kufuzu hatua inayofuata ya 16 bora.

'Lissu amevuliwa ili asigombee Urais' - Mashinji

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimedai kuwa hatua ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kuvuliwa Ubunge na kuzuiliwa kugombea Ubunge kwa miaka 5 inalenga kumzuia kutowania Urais kwenye Uchaguzi Mkuu kwa mwaka 2020.

Kauli hiyo ya CHADEMA imetolewa na Katibu Mkuu wa Chama Cha hicho, DR Vincent Mashinji wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya hatua ya maamuzi ya Spika kumvua Ubunge Tundu Lissu kwa kushindwa kuhudhuria Bungeni.
"Kuna ibara inamfunga Lissu kugombea ndani ya miaka mitano, na inambana hawezi kugombea Urais wa Tanzania kama hana sifa za kugombea Ubunge Tanzania, naomba tutafakari tukiwa tumebakiza mwaka mmoja kwenda Uchaguzi Mkuu 2020", amesema Mashinji.
"Muda wote ambao Spika anadai Lissu hajui alipo, Bunge limekuwa likimlipa mshahara, hili jambo si la kawaida, na watanzania wote wanajua Mama Samia Suluhu alikwenda kumsalimia Lissu Nairobi, na alienda kumpatia salamu za pole kutoka kwa Rais.", ameongeza Mashinji.
Mapema Ijumaa ya wiki iliyopita, Spika Job Ndugai alitangaza kumvua Ubunge Tundu Lissu kwa kile alichokidai kiongozi huyo kuwa na mahudhurio hafifu ndani ya Bunge.

Tutafungua ukurasa mpya dhidi ya Algeria - Amunike

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Emmanuel Amunike amesema kuelekea mchezo dhidi ya Algeria kesho, Stars haipaswi kufikiri matokeo ya nyuma baina na timu hizo
Amunike amesema licha ya Tanzania kushindwa kupata ushindi dhidi ya Algeria kwenye michezo ya nyuma, wanaweza kupata matokeo kwenye mchezo wa kesho kama hawatafanya makosa mengi
"Awamu iliyopita tulicheza na Algeria uwanja wa Taifa wakafanikiwa kurudisha mabao mawili na kutulazimisha sare ya 2-2. Baadae tukaenda Algeria wakatufunga mabao 7-0"
"Lakini matokeo haya yamepita, tunapaswa kujiandaa vizuri na tujiamini kuwa tunaweza kupata matokeo mchezo wa kesho," amesema Amunike
"Tunapaswa kujisahihisha na kutofanya makosa yaliyopelekea tuadhibiwe michezo iliyopita"
"Naamini Jumatatu tutafungua ukurasa mpya kati ya Tanzania na Algeria kwenye soka"
"Hatuwezi kutabiri nini kitatokea lakini naamini tutatoa upinzani mkali kwa Algeria"

Singida United yasajili mshambuliaji kutoka Ghana

Klabu ya Singida United FC imeanza rasmi usajili wake kuelekea msimu ujao kwa kumnasa mshambuliaji Herman Frimpong kutoka nchini Ghana akisaini mkataba wa miaka mitatu.

Frimpong mwenye umri wa miaka 22 ameshatua nchini Tanzania na amekabidhiwa jezi namba 14.

Maelfu ya Watanzania wamuombea Rais Magufuli



Na  Ferdinand Shayo,Arusha.

Maelfu ya Watanzania wamefanya maombi ya kumuombea Rais wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli pamoja na Viongozi wa serikali ili kuendeleza nguvu katika ujenzi wa Tanzania mpya ili kufukia uchumi wa Viwanda kama ilivyo ndoto ya Rais.


Mji wa Arusha umefurika maelfu ya watu kutoka ndani na nje ya mkoa wa Arusha pamoja na mikoa ya Kilimanjaro,Manyara,Singida,Dodoma ambao wamekusanyika kwa ajili ya kuiombea serikali  na Watanzania kwa ujumla.

Mkurugenzi Msaidizi wa Redio  Safina ,Hellen Lema amesema kuwa maombi hayo yanalenga kuomba Mungu azidi kumpa nguvu Rais Magufuli ili aweze kuwatumikia vyema Watanzania  na taifa la Tanzania lizidi kubarikiwa na kusonga mbele kiuchumi.

Mchungaji Pascal Thomas  amesema kuwa maombi hayo ya toba  dhidi ya maovu mbalimbali na kuhamasisha watu kumcha Mungu na kuondokana na uovu pamoja na kuwaombea viongozi.

Kwa upande wao wananchi Ester Mremi na  Joel Molel walioshiriki katika maombi hayo wameeleza umuhimu wa kuliombea taifa ili kuwa na muelekeo chanya wa kimaendeleo na kufungua milango ya kiuchumi ili waweze kufanikiwa.

BREAKING: CHADEMA WATOA TAMKO, TUNDU LISSU KUVULIWA UBUNGE..

Bonyeza play hapa chini kutazama zaidi pia tembelea app hii kila Mara kusoma habari mpya

Polepole Awapa Makavu Wanachama CCM....."Usitumie uongozi kama mali yako"

Katibu  wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Humphrey Polepole amesema ugonjwa mkubwa ndani ya CCM ni ubinafsi na kuwataka kuacha kupendekeza wagombea ambao wananchi hawawataki.

Aidha aliwataka viongozi wa chama wakiwemo mabalozi wa nyumba 10 kuacha kupanga safu za watu wanaowataka badala yake wahakikishe wanasimamia utaratibu.

Polepole alitoa maaelekezo hayo kwa makamisaa nchini kote kukisema Chama cha Mapinduzi kinachofanya kazi zake chini ya Rais John Magufuli ili wananchi waelewe .Aliyasema hayo jana Jijini Arusha katika kikao maalumu cha kupokea Ilani ya Uchaguzi wa CCM 2015/2020 katika kipindi cha robo tatu ya mwaka wa fedha Julai 2018 hadi Machi 2019.

Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi alisema anayepanga safu, aliyepangwa katika safu, kanuni za chama zinatoa adhabu kwa wale wote waliosababisha ukiukwaji wa uchaguzi au uteuzi wa wagombea

“Chama hakiangalii mtu kwa sura, mtatandikwa adhabu kali, uongozi ni dhamana usitumie uongozi kama mali yako na wale wabaya nawaambia acheni kupanga safu na tunawakata wale wote wasioheshimu maadili ya chama…

"Acheni kupanga safu za uongozi na nitawasubiri kwenye sekretarieti nitahangaika na wewe ulalo ulalo hadi kieleweke kura hazipigwi na viongozi wa CCM zinapigwa na wanachama wa CCM hivyo achene mambo yenu,” alisema.

Alisema kwenye serikali za mitaa, vijiji na vitongoji wekeni watu wanaokubalika na kama mnaona hawakubaliki kata weka wengine na mwaka kesho kwenye udiwani, madiwani wa CCM wafanye mikutano katika kata zao na wasiofanya mikutano wote watajulikana.

Polepole alisema Tanzania imepata bahati ya kuwa na Rais wa kipekee kwani Rais Magufuli amevunja historia nchini katika kipindi cha mwaka mmoja na miezi sita rais amejenga hospitali za wilaya 67 na vituo vya afya 353 nchi nzima.

Alisema yapo mengi mazuri Rais Magufuli amefanya ikiwa ni pamoja na kutoa ndege yake kwa ajili ya wananchi kuipanda na amenunua ndege kubwa mbili mpya, ujenzi wa bwawa kubwa la kufua umeme wenye uwezo wa kuvuna megawati za umeme zaidi ya 2000.

Usajili CAF hadi Julai 10

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kuwa dirisha la usajili wa CAF (bila faini) litafungwa rasmi Julai 10 2019 ikiwa ni siku 10 zaidi ya tarehe iliyotangazwa awali ambayo ilikuwa leo Juni 30

Ratiba ya AFCON 2019 leo

Mashindano ya AFCON2019 kuendelea leo nchini Misri kwa mechi za mwisho hatua ya makundi kupigwa.


MECHI ZOTE TUTAZIRUSHA LIVE HAPA HAPA USIKOSE

Donald Trump Kawa Rais wa Kwanza wa Marekani Kukanyaga Ardhi ya Korea Kaskazini Leo....Tazama Picha

Rais Donald Trump amekuwa rais wa kwanza wa Marekani kukanyaga ardhi ya Korea Kaskazini.

Trump amekutana leo na Kim Jong-un, kiongozi wa Korea Kaskazini katika mpaka usiokuwa wa kijeshi wa Korea Kaskazini na Korea Kusini, ambapo Trump amevuka mstari wa mpaka huo na kukanyaga ardhi ya Korea Kaskazini.

Baada ya kuvuka mstari unaoashiria mpaka wa nchi mbili hizo jirani, Trump amesema, "Hii ni fahari kubwa kwangu, Sikutaraji. Kuuvuka mstari huu ni jambo kubwa kwangu."

Trump ameambatana na Rais wa Korea Kusini, Moon Jae-in katika safari yake hiyo. Hii ni katika hali ambayo Trump awali alikuwa ametangaza kwamba hatokutana na Kim Jong-un katika safari yake ya Peninsula ya Korea.
Kiongozi wa Korea Kaskazini kwa upande wake amesema, "Trump amekuwa rais wa kwanza wa Marekani kuingia katika nchi yetu. Hatua hii inaashiria azma ya kufuta uhasama wa nyuma, na kufungua ukurasa mpya."

Rais wa Marekani na kiongozi wa Korea Kaskazini wamekutana mara mbili nchini Singapore na Vietnam, lakini vikao hivyo havijakuwa na tija, kwani Washington imeendelea kuiwekea Pyongyanga vikwazo, huku Pyongyanga nayo ikiendelea kufanyia majaribio makombora yake.
Trump akivuka mpaka na kukanyaga ardhi ya Korea Kaskazini
Baadaye wakapata muda wa kuongea na waandishi wa habari

Singida United yaiga usajili wa Simba

Klabu ya soka ya Singida United imetangaza kuwa itaanza kutangaza rasmi usajili wake leo Juni 30 kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania bara.

Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, klabu hiyo imesema kuwa kunzia Juni 30, saa 6:00 mchana itakuwa ikitangaza mchezaji mmoja.
Mfumo huo umekuwa ukitumiwa na Simba katika usajili wa kujiandaa na msimu ujao, ambapo imekuwa ikitangaza wachezaji wake kila siku majira ya saa 7:00 mchana, na mpaka sasa imeshaongeza mikataba na wachezaji wa msimu uliopita pamoja na usajili mpya wa wachezaji watatu wa Kibrazil.
Wachezaji watatu wapya waliosajiliwa ni pamoja na  beki Tairone Santos da Silva (30) aliyetia saini ya miaka 2 akitokea Atlético Cearense FC ya nchini kwao Brazil, mwingine ni beki wa kati na kiungo mkabaji, Gerson Fraga Vieira (26) ambaye amesaini mkataba wa miaka 2 akitokea klabu ya ATK FC ya India pamoja na mshambuliaji Wilker Henrique da Silva ambaye amesaini mkataba wa miaka 2.
Singida United pia imetangaza tarehe ya kuanza kambi rasmi ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu kesho Julai 1, ambapo kambi hiyo itafanyika mjini Singida.

TFDA yatoa neno mayai yenye viini viwili yaliyozua hofu

MAMLAKA ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) imewatoa hofu wananchi juu uwepo wa mayai yenye viini viwili na kusema kwamba hayana madhara yoyote.
Wakati TFDA wakisema hayo tovuti inayofuatilia usalama wa mayai ya ‘Egg Safety Center’ inaeleza kuwa viini viwili katika yai moja si jambo la kawaida sana ‘unsual’ na kutokea kwa viini viwili kunaweza kuhusishwa na usalama wa chakula.
Kauli hiyo ya TFDA imekuja baada ya kusambaa video ya dakika 1:19 inayonyesha kijana anayeuza mayai ya kuchemsha yenye viini viwili na hivyo kuzua hofu kwa walaji.
Katika video hiyo kijana muuza mayai anaonekana akiwa na vijana wengine wawili ambao walionyesha kuingiwa hofu baada ya kumenya yai moja walilonunua na kukuta lina viini viwili. Kijana huyo muuza mayai alisema mayai hayo yote yana viini viwili na kumenya jingine ambalo nalo lilikuwa hivyo hivyo.
Alidai mayai hayo wanachukua kutoka kampuni ya Interchic ingawa wao hajui hasa chanzo cha kuku wanaotoa mayai hayo.
“Haya tunachukua Interchic lakini sijui yanapotoka ila ni lazima yawe na viini viwili na yanatoka kwa kuku chotara” aliwaeleza wateja wake kijana huyo muuza mayai.
Katika kutaka kudhibitisha kama jambo hilo ni kweli kijana mteja alitaka limenywe yai jingine ili kuhakikisha endapo nalo lina viini viwili ambapo baada ya kumenya na kukata vilionekana.
“Haki ya Mungu haya ndio mayai ya kutengeneza, kwa kweli mtatuua uwii’, alisikika kijana mnunuzi akisema.
Baada ya video hiyo kusambaa na kuzua mjadala kwenye mitandao mbalimbali ya jamii hasa katika makundi ya whatsapp, Mtanzania Jumapili liliwatafuta TFDA kupata ufafanuzi juu ya hofu hiyo.
Ofisa Uhusiano wa TFDA, Gaudensia Simwanza alisema mayai yenye viini viwili hayana shida yoyote.
“Ukifuatilia hiyo ‘clip’ na ukienda kufatili kule yanakotoka wanaweza kukueleza kwanini mayai yote yametoka hivyo.
“Wao wanajihusisha na utotoleshaji vifaranga, wanapototolesha wanapoona mayai yana viini viwili, hayafai kutotolesha vifaranga hivyo wanaweka pembeni yanauzwa kwa hiyo hamna ‘ishu’ hapo” alisema Gaudesia .
MTANZANIA Jumapili liliwawatafuta Interchic kwa njia ya simu ambayo ilipokelewa na mtu aliyejitambulisha kwa jina la Bakita Kiongosi aliyesema kampuni hiyo haiuzi mayai bali inajihusisha na kuuza kuku, nyama, vifaranga na chakula cha kuku.
“Sisi hatuuzi mayai kwa mteja yoyote, sisi tunazalisha mayai ya kuku na kutotolesha vifaranga, hatuuzi mayai sehemu yoyote kwa mteja yoyote,” alisema Bakita.
MTANZANIA Jumapili pia liliwatafuta wazalishaji wengine wa vifaranga nchini ambao ni kampuni ya AKM Glitters Limited na kuzungumza na meneja masoko wake, Michael Joseph ambaye alisema mayai kuwa na viini viwili hilo jambo lipo na aina ya kuku ambaye anaweza kutoa mayai hayo ni aina ya Kroiler.
Hata hivyo Michael aliomba atumiwe kipande hicho cha video ili akione na alipokiona alirudi kwa mwandishi na kuendelea kueleza juu ya hali hiyo kuwa;
“Huyo kijana anasema anachukua kutoka kampuni ya Interchic sasa sijajua hayo mayai anayatoa kwa kuku wa aina gani maana kuna kuku aina nyingi, kuna kroiler, sasso, na kuku wa malawi
Akielezea kwa upande wao alisema kuwa wao wanahusika na hao kuku wa Kroiler na ndio kampuni pekee inayohusika na kuku aina hiyo nchini, lakini hawauzi mayai bali wanauza vifaranga.
Michael alisema huenda ni wateja ambao wanauziwa kuku hao ndio wanaozalisha mayai hayo. “Sisi hatuuzi mayai, bali tunauza vifaranga sasa wakianza kuwakuza na kufikia hatua ya kutaga ndio wanaweza kutaga mayai ya aina hiyo” alisema.
“Hata hivyo hiyo hutokea ‘by chance’ yaani ni sawa na kama mtu kupata watoto mapacha, yaani kuku anaweza kwa wiki akataga mayai matano na moja au mawili kati yao yakawa na viini viwili ndani” alisema
Alisema hiyo inawezekana mfugaji akawa anayakusanya na yanapofikia trei anayauza lakini si kwamba kuku kwa wiki nzima anaweza akawa anataga mayai hayo ya viini viwili.
Kuhusu kuwa na madhara, Michael alisema hayana madhara yoyote, ila kwa hayo ambayo yameonekana kwenye kipande hicho cha video hawezi kujua kwa kuwa hajui chanzo chake.
Aidha tovuti ya ‘Egg Safety Center’ imeeleza kwamba ni kawaida yai kuwa na kiini kimoja lakini kuna nyakati za nadra hutokea kuwa na viini viwili.
“Yai kuwa ni viini viwili ni jambo la nadra sana, kwa kawaida mayai yenye viini viwili hutagwa na kuku wadogo ambao mifumo yao ya uzazi haijawa kamilifu pia yanaweza kutagwa na kuku wakubwa wanaokaribia kufika ukomo wa kutaga mayai” unaeleza mtandao huo.
Mtandao huo unaeleza kwamba viini viwili katika yai moja si jambo la kawaida sana ‘unsual’ kutoka katika yai, na kutokea kwa viini viwili kunaweza kuhusishwa na usalama wa chakula.

Mwili wakutwa kichakani umekatwa miguu, mkono na Kiuno

Mtu  ambaye hajafahamika mara moja, amekutwa kichakani akiwa amefariki dunia huku baadhi ya viungo vyake vikiwa vimeondolewa.

Tukio hilo lilitokea katika kitongoji cha Nunga, Kata ya Ngogwa wilayani Kahama baada ya wananchi kuukuta mwili huo ukitoa harufu, huku viungo kama mkono, sehemu za siri na miguu vikiwa vimeondolewa na watu wasiojulikana wanaodaiwa kutekeleza mauaji hayo.

Ofisa Mtandaji wa Kata hiyo, Michael Magoyi, amesema  kuwa tukio hilo, kutokana na hali ya mwili, limetokea siku za karibuni chini ya wiki moja na wananchi walipogundua walitoa taarifa kwa mwenyekiti wa kitongoji hicho.

"Taarifa ya kuokotwa kwa mwili huo nilizipata kwa mwenyekiti wa kitongoji cha Nuja ambaye alidai kwamba alipelekewa taarifa hizo na mwananchi aliyefahamika kwa jina la Thomas Shaban. Baada ya kupokea taarifa hizo, nilifika eneo la vichaka kisha nikapiga simu polisi ambao walifika haraka na kuokota kiwiliwili hicho.

Magoyi alisema tukio hilo limezua taharuki miongoni mwa wananchi hasa baada ya watu waliofanya uhalifu huo kukata viungo mbalimbali vya mwili wa mtu huyo kisha kutoweka navyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi (ACP) Richard Abwao, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mtu huyo ambaye hajafahamika aliuawa na watu wasiojulikana kisha kutelekezwa porini.

Kamanda Abwao alisema baada ya wauaji kutekeleza tukio hilo, mwili huo waliusambaratisha kwa kuukata vipande vipande na kubakiza kichwa, mkono mmoja na kifua, huku viungo vingine kuanzia kiuno na miguu yake na mkono walitoweka navyo kwa lengo wanalofahamu wao.

Kutokana na tukio hilo, Abwao alisema Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga linaendesha msako ili kuwabaini watuhumiwa wa mauaji, huku akiwasihi wananchi lilikotokea tukio hilo, kuwa wepesi kutoa taarifa ili kudhibiti matukio ya namna hiyo.
Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list