Mkuu wa mkoa wa Katavi Juma Homera aapa kupambana na wanaotorosha dhahabu huku mpaka sasa watu wawili wakishikiliwa na jeshi la polisi kwa kununua dhahabu kinyume cha sheria mkoani humo.
RC Homera akiwa ziarani katika migodi mbalimbali ikiwemo dilifu ambao ni mgodi wa wachimbaji wadogo na mgodi mkubwa wa Katavi na Kapufi mining alieleza anachotaka wachimbaji wadogo wakauuze madini yao katika soko la madini la mkoa huo.
Homera alianza majukumu ya ukuu wa mkoa ikiwa soko limeshafanya biashara kwa kununua dhahabu gram 238, May 23/2019 jambo ambalo lilimfanya aanze kufatilia na kubaini dhahabu nyingi inayopatikana Mkoani Katavi inauzwa nje ya mkoa wa Katavi nakupelekea soko hilo kusua sua.
Kufuatia jambo hilo limemfanya Homera kuyafanyia kazi mapungufu ya soko hilo, mpaka sasa ununuzi na uuzaji wa madini ni Grams 6317.2 sawa na Kg 6 na Grams 317.2 yenye thamani ya Tshs.Million 519,155,127.56 zimenunuliwa kwa kipindi cha Mei na June 30/2019 na serikali kupata mrahaba (Royality7%) Tsh Milioni 36,340,858.92 na Service levy 0.3% Tsh.milioni 1,401,718.85.
Aidha ameimarisha mifumo ya Benk mbili katika soko hilo na ameendelea kuwabana mablokers na wanunuzi wenye leseni na wachimbaji mbalimbali kuhakikisha pia wanauza madini yao kwenye soko la mkoa ili tujenge uchumi wa Tanzania na kumuunga mkono Rais wetu Dkt.John Joseph Pombe Magufuli katika kuinua uchumi na miundombinu ya nchi hii kwa kulipa kodi.
No comments:
Post a Comment