Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Emmanuel Amunike amesema kuelekea mchezo dhidi ya Algeria kesho, Stars haipaswi kufikiri matokeo ya nyuma baina na timu hizo
Amunike amesema licha ya Tanzania kushindwa kupata ushindi dhidi ya Algeria kwenye michezo ya nyuma, wanaweza kupata matokeo kwenye mchezo wa kesho kama hawatafanya makosa mengi
"Awamu iliyopita tulicheza na Algeria uwanja wa Taifa wakafanikiwa kurudisha mabao mawili na kutulazimisha sare ya 2-2. Baadae tukaenda Algeria wakatufunga mabao 7-0"
"Lakini matokeo haya yamepita, tunapaswa kujiandaa vizuri na tujiamini kuwa tunaweza kupata matokeo mchezo wa kesho," amesema Amunike
"Tunapaswa kujisahihisha na kutofanya makosa yaliyopelekea tuadhibiwe michezo iliyopita"
"Naamini Jumatatu tutafungua ukurasa mpya kati ya Tanzania na Algeria kwenye soka"
"Hatuwezi kutabiri nini kitatokea lakini naamini tutatoa upinzani mkali kwa Algeria"
No comments:
Post a Comment