Waziri wa Nishati Medard Kalemani ameuagiza uongozi wa mkoa wa Shinyanga kuendelea kuwashikilia wakandarasi wa kampuni ya Angelique International LTD inayosambaza umeme wa REA katika maeneo ya Shinyanga vijijini na maeneo ya wachimbaji wadogo ya Mwakitiliyo hadi watakapomaliza kusambaza na kuwasha umeme katika vijiji vyote na kukaguliwa.
Waziri Kalemani ametoa kauli hiyo wakati akikagua utekelezaji wa maagizo aliyotoa akiwa katika ziara mkoani Shianyanga mwanzoni mwa mwezi huu na kubaini utendaji usioridhisha wa wakandarasi hao ambapo amedai kuwa kwa sasa ameridhika kidogo
Nao baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mwakitolyo ambacho kilirukwa na umeme wa REA wameipongeza serikali kwa kusikiliza malalamiko yao na kuyafanyia kazi kwa haraka na kwa kipindi cha wiki mbili wameshapata umeme kwa maelekezo ya waziri huku kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bi. Nyabaganga Daudi Taraba ambaye pia ni kuu wa wilaya ya Kishapu akimueleza waziri kalemani kuwa bado kasi ya kuunganisha umeme katika maeneo yaliyofikiwa ni ndogo kutokana na mwamko mdogo wa wananchi kulipia.
Katika hatua nyingine Waziri Medard Kalemani amemuagiza meneja wa Tenesco mkoa wa Shinyanga kusimamia ujenzi wa njia za umeme katika eneo la mwakitilyo ziunganishwe vizuri ili Mwakitolyo iwe kijiji cha mfano huku meneja wa Tanesco Shinyanga Fedigrace Shuma akidai kuwa changamoto kubwa inayofanya zoezi liende taratinu ni uchimbaji wa mashimo ya kusimika nguzo kutokana na eneo kuwa na mwamba mgumu.
No comments:
Post a Comment