Rais John Pombe Magufuli ameziagiza Wizara za Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kushirikiana kukamilisha ujenzi wa majengo mapya ya Chuo cha Ualimu cha Mpuguso Wilayani Rungwe.
Rais ametaka ujenzi huo uendane na thamani ya fedha zaidi ya Tsh. Bilioni 9 ambazo zimeshatolewa na serikali kwa ajili ya mradi huo.
Ametoa agizo hilo alipokuwa akizungumza na wananchi pamoja na Jumuiya ya wanachuo cha Ualimu Mpuguzo, ikiwa ni muda mfupi baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa majengo mapya ya chuo hicho ambayo yatagharimu Tsh. Bilioni 9.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa amesema serikali itatoa kibali cha kuajiri watumishi wapya zaidi ya 50,000 katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, kwa lengo la kuboresha utendaji kazi.
No comments:
Post a Comment