Bilionea na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) Mohammed Dewji ambaye pia ni muwekezaji wa club ya Simba kwa Tsh Bilioni 20 kama Simba, ametembelea club ya FC Porto ya nchini Urenona kujifunza mambo mbalimbali hususani kuhusiana na soka la vijana.
“Jana nilipata nafasi nzuri ya kujifunza nilipoitembelea @FCPorto ambapo niliweza kujua fursa za ushirikiano kwa kituo cha kukuzia vipaji cha Simba huko mbeleni. Tuna mengi ya kujifunza na kupata kutokana na uzoefu wa Porto FC. Natarajia kuimarisha mazungumzo yetu hivi karibuni”>>>MO Dewji
Hii sio mara ya kwanza kwa mfanyabiashara huyo kutembelea na kufanya mazungumzo na vilabu mbalimbali barani Ulaya, huku ikiripotiwa kuwa ni utaratibu wake wa kawaida kuendelea kufanya utafiti wa namna kuipeleka mbele zaidi club ya Simba, March 25 2017 MO Dewjialiripotiwa pia kufanya mazungumzo na club ya Juventus kuhusiana kukuza soka la vijana.
No comments:
Post a Comment