We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Thursday, May 2, 2019

Walichoandika Diamond, Vanessa Mdee, Idris Sultan na wengine kufuatia kifo cha Dkt. Mengi


Wasanii nchini wamezidi kutuma salamu za pole kufuatia kifo cha Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi kilichotokea usiku wa kuamkia leo. Chini ni baadhi ya  wasanii waliotuma salamu zao za pole kupitia mitandao.

Vanessa Mdee - What a loss. Poleni sana kwa ndugu jamaa na marafiki pamoja na kila mmoja aliyeguswa na msiba huu hakika ni wengi. Thankyou for your time, brilliance and the constant motivation 🙏 prayers up kwa familia na watoto wote 🙏 Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Mzee Mengi pahali pema. Praying for you sis J Mengi

Diamond Platnumz-  Dah! What a Sad news....May your Humbled Soul Rest in Paradise...🕯🙏🏻 🕯

Idris Sultan - Jana ilikuwa birthday ya Ruge na leo msiba wa Mengi. Another media tycoon is gone. Sina nafasi ya kuongezea kwenye huzini ambayo wote tunayo ila tukumbuke siku zake za mwisho na mkewe zilitupa wote furaha sanaaaa sio siri. It’s a life well lived. Innalillahi wainna ilaihi rajiun.

Mwijaku -  Binaaadamu hupimwa kwa mchango wake aliouacha kwenye jamii na sio umri alioishi kwenye jamii. Rest easy ,Reginald Mengi ,go and Dance with angels.Rest In Paradise. Pole J Mengi.

Chege Chigunda - Lala salama babaetu MENGI Mungu akuweke mahala pema peponi,poleni ndugu jamaa na marafiki wote mlo guswa na msiba huu mkubwa🙏 poleni sana wafanya kazi wa IPP Group Mipango ya Mungu haina makosa

Utakumbuka Dkt. Reginald Mengi amefariki dunia, kwa mujibu wa taarifa kutoka vyombo vya habari alivyokuwa anavimiliki. Mengi ambaye ni mmoja kati ya wafanyabishara wakubwa Tanzania amefariki usiku wa kuamkia leo Alhamisi akiwa Dubai.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list