We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Thursday, May 2, 2019

Makatibu Wakuu Tanzania na Uganda wasaini makubaliano


Mkutano wa Kuendeleza Mahusiano ya Mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na Uganda kwa ajili ya kurahisisha masuala ya kijamii, Kiuchumi na Kimazingira umemalizika Bukoba mkoani Kagera kwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Faraja Mnyepe na Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Mazingira wa Uganda Alfred Ollot kusaini makubaliano yaliyofikiwa.

Mkutano huo wa siku mbili ulimalizika juzi na kuwakutanisha Makatibu Wakuu wa nchi za Tanzania na Uganda kutoka Wizara zinazoshughulika na masuala ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mambo ya Nje, Mifugo na Uvuvi, Maji pamoja na Nishati.

Kabla ya mkutano huo, Wataalamu wa sekta zinazohusika kutoka nchi hizo mbili walikutana na kujadiliana namna bora ya kukabiliana na changamoto zinazozikabili nchi za Tanzania na Uganda katika eneo la Mpaka na baadaye kuwasilisha mapendekezo kwa Makatibu Wakuu kwa lengo la kujadiliwa kwa manufaa ya nchi hizo.

Baadhi ya mambo yaliyojadiliwa kwenye mkutano huo ni pamoja na Uimarishaji na Uthamini wa Mpaka wa Kimataifa wa Tanzania na Uganda, Mpango Kabambe wa Utunzaji Mto Kagera na Matumizi Endelevu ya Rasilimali za Bonde la Mto Kagera kati ya Tanzania na Uganda.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Faraja Mnyepe alizishukuru pande zote mbili za nchi za Tanzania na Uganda kwa kufanikisha kufikiwa makubaliano aliyoyaeleza kuwa yana lengo la kuleta manufaa kwa nchi za Tanzania na Uganda.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list