We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Thursday, May 30, 2019

TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO ALHAMISI

Dybala
Bayern Munich wamewasilisha dau la £80m kumsajili mshambuliaji wa Juventus na Argentina, mwenye umri wa miaka 25 Paulo Dybala. (Corriere dello Sport - in Italian)
Atletico Madrid wamewasilisha dau la £71m kumnunua beki wa klabu ya Leicester City na Uingereza Ben Chilwell, 22 lakini itakabliwa na ushindani mkali kutoka kwa klabu ya Manchester City. (Sun)
Kiungo wa kati wa Leiceste James Maddison, 22, anavutia hamu kutoka kwa Tottenham . (Mirror)
Ashley YoungHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Beki wa Manchester United na Uingereza Ashley Young, 33, huenda akaungana na mchezaji mwenza wa zamani Wayne Rooney katika klabu ya DC United inayocheza ligi ya Major league nchini Marekani.(Manchester Evening News)
Meneja wa Watford na Uhispania Javi Gracia, 49, ameorodheshwa miongoni mwa wakufunzi watano kuchukua mahala pake Rubi katika klabu ya Espanyol. (Marca - in Spanish)
Beki wa kushoto wa Lyon na Ufaransa Ferland Mendy, 23, anatarajiwa kujiunga na Real Madrid. (AS - in Spanish)
Matthijs de LigtHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Beki kinda wa Ajax na Uholanzi mwenye umri wa miaka 19 Matthijs de Ligt anaivutia klabu za Real Madrid. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Mshambuliaji wa Valencia na Uhispania Rodrigo Moreno, 28, na mshambuliaji wa klabu ya Girona Cristhian Stuani, 32, wanalengwa na Barcelona. (marca)
West Brom wamefanya mazungumo ya awamu ya pili na mkufunzi wa Wolfsburg na Ujerumani Bruno Labbadia, 53, huku usakaji wa mkufunzi mpya ukiendelea. (Express & Star)
Roberto MartinezHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Mkufunzi wa zamani wa Wigan na Everton Roberto Martinez, 45, hatochukua mahala pake kocha Ernesto Valverde iwapo atafutwa kazi.
Martinez ambaye ni raia wa Uhispania amehusishwa sana na ukufunzi wa Barcelona . (Mundo Deportivo - in Spanish)
Winga wa Manchester City na Uingereza Patrick Roberts, aliyehudumu msimu uliopita kwa mkopo katika klabu ya Girona nchini Uhispania anajiunga na klabu mpya iliopandishwa katika ligi ya Premia kwa mkopo katika kipindi cha msimu wa 2019-20.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 ameshiriki katika mechi moja ya ligi ya Premia akiichezea City.. (Telegraph)

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list