Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' itacheza mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya Nigeria au Zimbabwe kabla ya kuelekea nchini Misri kushiriki fainali za michuano ya AFCON 2019 zinazoanza nchini humo Juni 21
Stars imepanga kucheza michezo miwili ya kirafiki kabla ya kwenda Misri ikiwa tayari imethibitisha kucheza na wenyeji Misri Juni 13
Rais wa TFF Wallace Karia amesema wamefanya mazungumzo na timu za Nigeria na Zimbabwe huku Zimbabwe ikionekana kuwa tayari zaidi kujipima na Stars
Katika hatua nyingine, Stars itaweka kambi ya siku sita kwenye Hotel ya White Sands jijini Dar es salaam kabla ya safari ya kuelekea nchini Misri Juni 07
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Motisun Group Subhash Patel amesema White Sands itagharamia kambi hiyo ya siku sita ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika kuthamini ushiriki wa Tanzania kwenye michuano ya AFCON baada ya kusubiri kwa miaka 39
Wachezaji 39 ambao waliitwa na kocha Emmanuel Amunike wataingia kambini wiki hii na saba watapunguzwa kabla ya kikosi cha Stars kuondoka kuelekea Misri

No comments:
Post a Comment