We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Wednesday, May 29, 2019

"Sekta yetu ni ngumu" - Waziri Mkuu

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu waongeze kasi ili utendaji kazi serikalini uweze kufikia hatua nzuri.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo alipokutana na viongozi na watumishi wa ofisi yake na kufuturu nao pamoja kwenye makazi yake jijini Dodoma.
Ninawashukuru watumishi wote kwa ushirikiano mnaotupatia mimi pamoja na mawaziri wenzangu, makatibu wakuu wote watatu, Wakurugenzi mbalimbali na wakuu wa vitengo. Tunatakiwa tuongeze kasi ili tufikie hatua nzuri ya utendaji kazi serikalini”,amesema Waziri Mkuu
Aidha amesema utendaji kazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu ni mgumu kwa sababu unahusika na usimamizi wa shughuli za Serikali nzima na watendaji wote wa Serikali.
"Sekta yetu ni ngumu kwa sababu sisi ni wasimamizi wa Serikali na watendaji wote wa Serikali. Tuna wajibu wa kuwaunganisha watendaji wa wizara zote serikalini”, ameongeza Waziri Mkuu.
Sisi sote ni watumishi wa umma, kwa hiyo mchango wenu una maana kubwa na unachangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya Serikali nzima. Ninawapongeza kwa utumishi mwema na wenye uadilifu”.amesema Waziri Mkuu

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list