We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Thursday, May 2, 2019

RAIS MAGUFULI ‘AMPUKUTISHA’ PESA DIWANI – VIDEO

RAIS  Dkt John Magufuli ‘amempukutisha’ pesa kiasi cha shilingi laki tano, Diwani wa Inyala mkoani Mbeya baada ya diwani huyo kumuomba Rais awasaidie kumalizie ujenzi wa shule iliyopo eneo hilo, badala yake Rais alimtaka yeye kama diwani achangie pia katika ujenzi huo.

Tukio hilo limejiri leo Alhamisi, Mei 2, 2019 katika eneo la Inyala, Tarafa ya Tembela, Wilaya ya Mbeya Vijijini, wakati Magufuli aliposimama barabarani kuzungumza na wananchi hao.
Magufuli alimsimamisha diwani huyo (jina halijafahamika) na kumtaka aeleze shida za eneo hilo, diwani alianza kwa kumshukuru Rais Magufuli kwa miradi aliyoileta katika wilaya hiyo, ikiwemo Tsh Bil. 4, alizowapa kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya Afya.

Diwani alimweleza MAGUFULI kuwa katika ujenzi wa shule wana upungufu wa mabati bando 30, hivyo akamwomba awachangie.
Rais aliwaambia bando 30 ni chache hivyo yeye na Madiwani wenzake wakamalizie hizo bando 30. Rais alimuuliza yeye kama diwani anachangia kiasi gani, alipotaja laki 1, Rais akamkatalia alipotaja laki 2 Raisi alikataa pia, alipotaja laki 3 Rais akamgomea, mapaka alipotaja laki 4, Rais akamwambia atatoa laki 5 na yeye akakubali huku wananchi wakishangilia.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list