Leo Mei 1, 2019, ni kumbukumbu ya siku ya Kuzaliwa kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group, marehemu Ruge Mutahaba aliyeaga dunia Februari 26, nchini Afrika Kusini alikokuwa akipatiwa matibabu.
Katika Kijiji cha Kiziru – Bukoba mkoani Kagera, ambako ndiko alikozaliwa Ruge, leo imefanyika Misa ya shukrani kumkumbuka na kumuombea marehemu Ruge.
Katika ibada hiyo ya kutimiza miaka 49 ya Ruge iliyohudhuriwa na wanafamilia, ndugu na marafiki kijijini hapo, mwimbaji kutoka THT na aliyekuwa rafiki wa karibu na Ruge, Nandy amesema mirathi tosha aliyoachiwa na Ruge “Ni akili, strategy ya maisha, muziki wangu kiujumla ni mirathi tosha kwangu.’
Kwa upande wake, mtoto wa marehemu Ruge, Mwachi Mutahaba, amesema; “Nandy alikuwa na urafiki na baba yangu na nimeanza kumjua kupitia hivyo, Na pia kwa baba alikuwa ni msanii wa THT na alikuwa ni mpambanaji kwenye industry yagame, so nilikuwa namuheshimu.
“Kwa familia tumemfahamu Nandy kama rafiki wa baba yangu na ni mtu aliyekuwa anamuheshimu sana baba, sisi tumeamua kumheshimu na yeye kwa jinsi anavyotuheshimu sisi na baba yangu,” amesema Mwachi Mutahaba.
Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Januari Makamba kupitia akaunti yake ya Twitter ameandika;
“Ruge, leo ungetimiza miaka 49 ya hapa. Lakini umetuwahi kwenda kuanza maisha ya milele. Nakusalimu. Familia na marafiki wote wazima.
“THT itakuwa sawa. Uhakika wa safari ya kuja huko uliko unaendelea kunisaidia kuishi kwa amani, bila hofu ya mtu au jambo lolote. Endelea kupumzika. Kutoka Kijijini Kiziru Bukoba nyumbani kwao mpendwa wetu #RugeMutahaba ambako ilifanyika Misa fupi ya Shukrani iliyoandaliwa na familia yake.”
No comments:
Post a Comment