Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba Crescentius Magori amezitaka timu zinazowania wachezaji wa Simba zifuate taratibu kwa kuandika barua rasmi kwani timu hiyo haitakuwa tayari kushirikiana na wanaotumia njia za mkato
Magori amesema baadhi Mawakala na viongozi wa timu nyingine wamekuwa wakipiga simu wakiwaulizia baadhi ya wachezaji wa Simba
Amesema Simba kwa sasa inaendeshwa kisasa, wanapaswa kuandika barua rasmi kwenda klabuni
"Klabu yeyote inayohitaji mchezaji wetu waandike barua, hatutashirikiana na watu wasiofuata utaratibu," amesema Magori
"Kwa sasa tunaendesha timu yetu kisasa kwa weledi hivyo hatutarajii kuona mtu anapiga simu sijui wakala, sijui kocha mambo hayo ya kizamani yamepitwa na wakati kwa Simba Sc"
"Utaratibu huo sisi hatuutaki"
Inaelezwa kuna timu kubwa barani Afrika zinawawania nyota wa timu hiyo waliyofanya vizuri kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika ambayo Simba ilitolewa hatua ya robo fainali
Ofa nyingi zinamiminika kumtaka kinara wa mabao wa timu hiyo Meddie Kagere pamoja na kiungo Clatous Chama
Wachezaji hao bado wana mikataba ya klabu ya Simba

No comments:
Post a Comment