Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba wamewasili salama wilayani Kibaha na kupokelewa na idadi kubwa ya mashabiki wa timu hiyo
Baada ya Simba kuwasili, Kibaha ilizizima kwa shangwe na furaha ya mashabiki waliojitokeza kufurahia ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania ambao Simba walikabidhiwa mkoani Morogoro jana
Simba iko njiani kurejea jijini Dar es salaam ambapo shangwe kubwa zaidi itarindima mtaa wa Msimbazi, yalipo Makao Makuu ya timu hiyo

No comments:
Post a Comment