Bodi ya ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imekiri kuwepo kwa mkanganyiko wa takwimu uliopelekea Kagera Sugar kuwekwa kimakosa katika nafasi ya 19 ya msimamo wa ligi na hivyo kushushwa daraja pamoja na African Lyon
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura amesema wamesahihisha makosa hayo na watamuwajibisha aliyesababisha upotoshaji wa takwimu hizo
Sasa ni rasmi Stand United ndio itakayoshuka daraja pamoja na African Lyon wakati Kagera Sugar itacheza mchezo wa mtoano dhidi ya Pamba Fc na Mwadui Fc itachuana na Geita Gold kusaka nafasi ya kubakia ligi kuu au kupanda daraja kwa timu za daraja la kwanza

No comments:
Post a Comment