Kampuni ya Africa Media Group Ltd inayomiliki vituo vya Channel Ten na Radio Magic Fm imekabidhiwa vifaa vipya vya kisasa vyenye thamani ya Shs. Milioni 200.
Vifaa hivyo ahadi iliyotolewa na M/Kiti wa Chama cha Mapinduzi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipotembelea vituo hivyo wakati wa maadhimisho ya miaka 42 ya CCM mwaka huu .
Akikabidhi vifaa hivyo mbele ya Wafanyakazi na Uongozi wa Kampuni ya Amgl kwa Niaba ya Rais John Magufuli na viongozi wengine wa chama cha Mapinduzi, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole amesema Rais ametimiza ahadi aliyoitoa kwa wakati, hivyo amewataka wafanyakazi hao kutumia vyema vifaa na kutimiza wajibu
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa vyombo vya habari vinavyomilikiwa na CCM, Bw. Ernest Sungura na Afisa Mtendaji Mkuu wa AMGL bwana Jaffar Haniu wamempongeza Rais. John Pombe Magufuli kwa kutimiza ahadi aliyoitoa baada ya kusikiliza kilio cha wafanyakazi.
No comments:
Post a Comment