Amunike jana alitangaza majina ya wachezaji 39 watakaounda timu ya Taifa kwa ajili ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), zilizopangwa kuanza Juni 21 hadi Julai 19 nchini Misri.
Miongoni mwa wachezaji walioitwa katika kikosi hicho yumo beki huyo wa Simba ambaye amekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu baada ya kuumia goti.
Kapombe ambaye ameanza mazoezi ya viungo (gym) aliumia goti akiwa katika kambi ya Taifa Stars nchini Afrika Kusini, iliyokuwa ikijiandaa kwa mchezo dhidi ya Lesotho uliokuwa wa kuwania kufuzu Fainali za AFCON 2019. Taifa Stars ilifungwa bao 1-0.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Amunike alisema Kapombe ni mchezaji mzuri ana uzoefu wa mashindano ya kimataifa, hivyo anaweza kumtumia katika mechi za kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika Kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zilizopangwa kuanza Januari hadi Februari nchini Cameroon, mwakani.
“Nimeita idadi kubwa ya wachezaji akiwemo Shomari Kapombe kwa kuwa tuna mashindano mawili ya AFCON na CHAN, yeyote kati yao ana nafasi ya kucheza endapo atakuwa fiti,” alisema Amunike.
Nafasi ya beki wa kulia anayocheza Kapombe ina mabeki wengine wawili ambao ni Andrew Phillip wa Mbao na Hassani Kessy wa Nkana Red Devils ya Zambia.
Pia alisema amemuita kwa mara ya kwanza kinda wa Serengeti Boys, Kelvin John ‘Mbappe’ ili kumpa uzoefu katika mashindano ya kimataifa baada ya kucheza kwa kiwango bora katika Fainali za Kombe la Mataifa Afrika kwa vijana (AFCON).
Alisema ametoa nafasi kwa wachezaji vijana ili kuwajengea uwezo mzuri wa kupata maandalizi ya kutosha kwa mashindano ya kimataifa na baadaye warithi nafasi za wachezaji wakongwe ambao watastaafu soka.
“Tumefanikiwa kufuzu AFCON lakini tunataka kwenda kushindana kwahiyo tutahakikisha tunapata mechi ngumu za kirafiki ingawa hatutaangalia sana matokeo, kikubwa ni kuangalia kasoro na ubora,” alisema Amunike.
Kocha na mchambuzi wa soka Kennedy Mwaisabula alisema kuitwa kwa Kelvin ni njia ya kumjengea uwezo wa kushindana na kupata uzoefu katika michuano ya kimataifa.
“Kuitwa Kelvin haimaanishi anakwenda kucheza moja kwa moja, hata Ronaldo de Lima wakati anaitwa timu ya Brazil alikwenda Kombe la Dunia kuangalia nini ambacho wenzake wanafanya, lakini baadaye yeye ndiyo alikuja kuwa tegemeo,” alisema kocha huyo wa zamani wa Yanga.
Taifa Stars inatarajia kuanza mazoezi kujiandaa na Fainali za AFCON Juni Mosi na inatarajiwa kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Misri na Nigeria. Wachezaji 32 kati ya 39 ndiyo watakwenda Misri.
Kikosi kamili, Aishi Manula (Simba), Metacha Mnata (Mbao), Claryo Boniface (U-20), Suleman Salula (Malindi FC), Aron Kalambo (Prisons), Hassan Kessy (Nkana FC), Vicent Philipo (Mbao), Shomari Kapombe (Simba), Gadiel Michael (Yanga), Abdi Banda (Baroka),
Ally Mtoni (Lipuli), Mohammed Hussein (Simba), Agrey Morris (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Erasto Nyoni (Simba), David Mwantika (Azam), Ally Ally (KMC), Kennedy Wilson (Singida), Feisal Salum (Yanga), Himid Mao (Petrojet), Mudathir Yahya (Azam), Yahya Zaydi (Ismailia).
Jonas Mkude (Simba), Ibahim Ajibu (Yanga), Fred Tangaru (Lipuli FC), Frank Domayo (Azam FC), Shabani Chilunda (Tenerife AFC), Shiza Ramadhan Kichuya (ENPPI), Simon Msuva (Al Jadida), Rashid Mandawa (BDF Xi), Mbwana Samatta (KRC Genk).
Pia wamo Thomas Ulimwengu (JS Saoura), John Bocco (Simba), Farid Mussa (Teneriffe), Ayoub Lyanga (Coastal Union), Kassim Hamis (Kagera Sugar), Miraj Athumani (Lipuli), Kelvin John (U-17) na Adi Yusuph (Solihull Moors).

No comments:
Post a Comment