Rais Magufuli amesema serikali inapata fedha za kuweza kutekeleza miradi mikubwa kutokana imeweza kupambana na ufisadi.
Ametoa kauli hiyo wakati akiendelea na ziara yake mkoani Mbeya ambapo leo ataweka jiwe la Msingi la ujenzi wa nyumba za walimu, mabwenu na maabara katika Chuo cha Ualimu Mpuguso na kuzungumza na wananchi wa Tukuyu.
"Fedha kwa ajili ya kutoa elimu bure kwa watoto wetu wakiwemo watoto wa Kyela,Kila mwezi zinatolewa bilioni 23.86 mishahara tulikuwa tunasubiri mpaka miezi miwili saa nyingine,leo tarehe 19 wafanyakazi wote wana mishahara."
Ameendelea kwa kusema, "Mnaweza kujiuliza hizi fedha zinatoka wapi,tumewabana mafisadi ndio maana zimepatikana hizi fedha..ni kazi ngumu kwa sababu wala rushwa na mafisadi hawana alama kwenye uso unaweza kukuta ni CCM, CHADEMA au hana chama lakini ni fisadi kweli kweli".
No comments:
Post a Comment