Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameendelea kusisitiza kuwa Tanzania na nchi jirani wataendelea kushirikiana kwani ni ndugu na wanahitajiana.
Ametoa kauli hiyo katika ziara yake mkoani Mbeya ambapo ameeleza kuwa WaAfrika wanapaswa kuwa wamoja na kuishi kwa ushirikiano.
"Sisi na Malawi ni ndugu na nilazima tushirikiane katika masuala mbalimbali ya kutuletea maendeleo, na ndiyo maana kuna wakati tunachonganishwa na mabeberu, na sisi baadhi yetu tunakubali kuwa vibeberu vidogo vidogo. Tusikubali kuchonganishwa, lazima tusaidiane." amesema Rais Magufuli.
Utakumbuka April 24 mwaka huu Rais Magufuli aliwasili nchini Malawi na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Malawi Prof. Arthur Peter Mutharika katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kamuzu uliopo Lilongwe nchini Malawi na kuanza ziara yake ya siku mbili.
No comments:
Post a Comment