Mfalme Akihito alitangaza kuachia madaraka katika hotuba yake ya mwisho rasmi kwa watu wa taifa lake, huku akiwashukuru Wajapani kwa msaada wao wakati wa utawala wake wa miaka 30 ulioshuhudia mafanikio na changamoto.
Mfalme Akihito wa Japan alifanya maombi mbele ya Mungu wa Jua "Shinto” siku ya leo, huo ukiwa ni mwanzo wa hatua za kumalizika kwa utawala wake wa miaka 30.
Mfalme huyo mwenye umri wa miaka 85 alivaa vazi la kijadi alipokwenda Hekalu la Kashikodokoro kuielezea miungu kuhusu kustaafu kwake. Mfalme Akihito atamwachia mamlaka mwanawe Naruhito.
Akihito ndiye wa kwanza wa Japan kuachia madaraka katika muda wa karne mbili. Alisema ilikuwa ni heshima kubwa kwake kutekeleza majukumu yake huku watu wa Japan wakiwa na imani kamili kutokana na uongozi wake.
No comments:
Post a Comment