We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Monday, April 1, 2019

Tiboroha apitishwa na TFF kugombea uenyekiti Yanga


Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka hapa nchini (TFF) chini ya Mwenyekiti wake, Ally Mchungahela imempitisha Dk Jonas Tiboroha kuendelea na mchakato wake wa kugombea nafasi ya Uenyikiti wa klabu ya Yanga.

Tiboroha alisimama kuendelea na kampeni za uchaguzi wa kugombea nafasi hiyo baada ya uchaguzi wa kwanza kusimamishwa na wanachama ambao walifungua kesi katika mahakama mbalimbali hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za TFF, Mchungahela amesema kuwa wagombea wa nafasi ya uenyekiti wanaruhusiwa kuendelea kugombea nafasi hizo katika uchaguzi mpya wa klabu hiyo ambao sasa mepangiwa kufanyika Mei 5 ya mwaka huu.

"Wagombea ambao walikuwa na mchakato wa kugombea nafasi katika ule uchaguzi wa awaki wataendelea kama kawaida wakiungana na wagombea wapya ambao wataanza kuchukua fomu kuanzia Aprili 2.

"Uchaguzi mpya wa Yanga sasa utafanyika Mei 5, mwaka huu na kutakua na siku za kuchukua fomu, usahili wa wagombea na mambo mengine," amesema Mchungahela.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list