Na Ahmad Mmow, Nachingwea.
Chama Cha Mapinduzi(CCM), mkoa wa Lindi kimeziomba taasisi za serikali zenye dhamana ya kufatilia ubora na matumizi ya fedha zinazotumika katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo mkoani humu.
Wito huo ulitolewa jana na mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Lindi, Fadhily Mohamed kwenye kongamano la maadili lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa shule ya sekondari Nachingwea, iliyopo mjini Nachingwea.
Mohamed alisema kunaumuhimu mkubwa wa taasisi hizo kufuatilia matumizi ya fedha na ubora wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa mkoani humu ili kuepuka hasara zinazosababishwa na ufisadi unaofanywa na baadhi ya watumishi wasio waadilifu.
Alisema nijambo la kusikitisha kuona baadhi ya miradi ya maendeleo imekwama au kutumia fedha nyingi kuliko ukubwa wa miradi inayotekelezwa.Hali ambayo inachangia kukwamisha mipango ya serikali ya kuwahudumia na kuwapelekea maendeleo wananchi.
"Mfano ni fedha zilizotolewa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya cha Kilimarondo zinalingana na zilizotolewa kwa ujenzi wa kituo cha afya cha Mpengere. Lakini Mpengere kimefikia hatua mzuri, tofauti na Kilimarondo," alisema Mohamed.

No comments:
Post a Comment