Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu leo amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia masula ya Afrika Mashariki na Sudan Balozi Makila James.
Katika kikao hicho lengo kuu lilihusu ushirikiano baina ya nchi ya Tanzania na Marekani juu ya kuongeza idadi ya watu wanaofahamu hali zao za maambukizi ya VVU, ili kufikia lengo la kidunia ni kutokomeza maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi ifikapo mwaka 2030.
Katika kufikia lengo hilo Shirika linaloshughulikia mambo ya Ukimwi UNAIDS pamoja na shirika la afya la duniani (WHO) waliweka malengo ya kuanza 909090, yaani 90 ya kwanza ni asilimia 90 ya watu wanaokadiriwa kuishi na maambukizi ya ukimwi wawe wamepima na kutambua jali zao za maambukizi;
Asilimia 90 ya pili ni asilimia 90 ya hao wanaojua hali zao za maambuki wawe kwenye mpango mpango wa kupatiwa dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi (ARVs); 90 ya tatu asilimia 90 ya watu wanaotumia dawa za kufubaza dawa virusi vya Ukimwi wawe na kiwango na chini cha virusi katika miili yao.
Mwisho
No comments:
Post a Comment