Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi amesema dawa ya kuongeza nguvu za kiume ambayo haina kemikali ipo lakini serikali badi haijatangazwa rasmi na kuanza kutumika.
Ameeleza hayo leo Bungeni wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Ulanga (CCM), Godluck Mlinga aliyetaka kujua iwapo dawa ambazo zimekuwa zikitumika kwa kuongeza nguvu za kiume zina madhara..
Waziri Dtk. Mwinyi akijibu kwa niaba ya Waziri Afya amesema sababu za watu kupungukiwa nguvu za kiume ziko nyingi ikiwemo ugonjwa wa kisukari na msongo wa mawazo, lakini akasema Serikali ilishabaini uwepo wa dawa kwa ajili ya wanaume ambazo hazina kemikali kwa watumiaji.
No comments:
Post a Comment