Mara baada ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG, Prof. Mussa Assad kutoka ripoti yake ya Fedha za Mamlaka ya Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018, kumekuwa na maoni mbalimbali kutoka vyama vya upinzani nchini.
Leo Mwenyekiti wa ACT Wazalendo katika Mkoa wa Dar es Salaam, Soud Salimu amesema licha ya Jiji la Dar es Salaam na manispaa zake kupata hati safi kama ilivyo katika ripoti ya CAG, bado kuna maeneo yanahitaji kutupiwa jicho kwa kuwa kuna ubadhirifu wa kutisha.
Salimu amesema ripoti ya CAG inaonyesha kuna malipo yamefanywa bila kuidhinishwa na mamlaka husika ambapo mamlaka 17 zimefanya malipo ya TZS 1,033,321,426 ambapo miongoni mwa hizo ni kutoka mkoa wa Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment