Habari kubwa katika soka leo ni kuhusiana na taarifa zilizoripotiwa na mitandao mbalimbali ya habari za michezo barani Ulaya kuhusiana na kifo cha mchezaji wa timu ya taifa ya Czech Republic na club ya Aytemiz Alanyaspor ya Uturuki Josef Sural.
Sural mauti yamemkuta katika ajali akiwa katika mini-bus aliyokuwa anasafiria na wachezaji wenzake baada ya mechi waliyokuwa wanacheza ugenini, Sural akiwa na wachezaji wenzake alifariki akiwa hospitalini walipokuwa wamekimbizwa na wenzake kwenda kupatiwa matibabu baada ya ajali hiyo.
Wachezaji saba wa Aytemiz Alanyaspor akiwemo Sural walikodi VIP mini-bus baada ya kucheza game ya ugenini na kujikuta wakitoka sare ya 1-1 dhidi ya Kayserispor, Sural na wenzake walipata ajali kilometa 5 baada ya kuanza safari wakiwa Kusini mwa pwani ya Alanya nchini Uturuki.
Inaelezwa kuwa baada ya game hiyo baadhi ya wachezaji wa Aytemiz Alanyaspor na benchi la ufundi walirudi na basi la timu huku wengine wakitumia magari yao binafsi na wengine saba akiwemo Sural walikodi VIP mini-bus yao kurejea makwao baada ya mchezo, Sural amefariki akiwa na umri wa miaka 28 na ameichezea timu ya taifa ya Czech kwa muda mrefu.
No comments:
Post a Comment