We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Tuesday, April 9, 2019

Mbunge CHADEMA Aivaa CCM

Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Zainabu Bakari Mussa amedai CCM hawana ubavu ndiyo maana hawawezi kuruhusu tume huru ya uchaguzi.

Zainabu amesema ili CCM wajiamini na kujipima kwa wananchi kama wanakubalika, waweke tume huru ya uchaguzi na kwamba Watanzania watakilaza chama hicho ‘kifo cha mende’.

Akichangia jana Jumatatu Aprili 8, 2019 katika hotuba ya Waziri Mkuu kwa makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka 2019, Zainabu amesema uwanja wa siasa kwa sasa hauko sawa.

Amesema vyama vya siasa vimeminywa na kukosa uhuru wa kufanya siasa zao wakati CCM kunaendelea kufanya siasa, hivyo akaomba katiba mpya aliyosema itajibu yote.

"Kama mnabisha leo hii tuweke makubaliano ili iundwe tume huru ya uchaguzi muone kama 2020 hamtakufa kifo cha mende, narudia mtakufa kifo cha mende kwani Watanzania wa sasa wanaona," amesema Zainabu.

Mbunge huyo amelalamikia suala la kile alichokiita uonevu na ukandamizwaji wanaofanyiwa wapinzani.

Amesema vyama vya upinzani kwa sasa havifanyi siasa kama inavyowapasa wanasiasa, badala yake wanaminywa huku wenzao wa chama tawala wakiruhusiwa.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list