Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amewasili usiku wa kuamkia leo Jumatano kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na ataungana na kikosi cha Yanga kinachoondoka kesho kuelekea jijini Mwanza
Zahera alikuwa DR Congo kutimiza majukumu ya timu ya Taifa ambapo wamefanikiwa kukata tiketi ya kutinga fainali za AFCON 2019 kama ilivyo kwa Tanzania
Yanga inatarajiwa 'kukwea pipa' kesho Alhamisi kuelekea Mwanza tayari kwa mchezo wa robo fainali kombe la Azam (ASFC) dhidi ya Alliance Fc
Mchezo huo utapigwa katika uwanja wa CCM Kirumba, Jumamosi, March 30 2019
No comments:
Post a Comment