We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Wednesday, March 27, 2019

TETESI ZA USAJILI NDANI YA KLABU YA SIMBA LEO JUMATANO

USAJILI : Simba sasa ni sifa,Hiyo mashine inayoshuka Kagere kitaeleweka
Simba imenogewa kimataifa ndiyo kauli unayoweza kuisema kwa sasa kwani mipango ya kuwa na jeshi imara kwaajili ya msimu ujao wa michuano ya ndani na nje imeanza kuonekana.
Inaelezwa kuwa Simba tayari wameanza mchakato wa kuinasa mashine hatari ya Kinyarwanda inayocheza soka la kulipwa nchini Kenya katika klabu ya Gor Mahia.

Mchezaji huyo ni Jack Tuyisenge ambaye wakiwa Gor Mahia walikuwa na Combination moja hatari sana na Meddie Kagere ambaye kwasasa yuko katika kikosi cha Simba.
Taarifa zinaeleza kuwa mchezaji huyo kwasasa yupo katika jiji la Dar Es Salaam huku ikielezwa kuwa huenda akafanya mazungumzo na klabu ya Simba ambayo inataka kuongeza na kuimarisha jeshi lake.

Mbali na hayo baadhi ya Taarifa zinaeleza kuwa nyota huyo kuwa anafukuziwa na baadhi ya vilabu vikubwa barani Afrika ikiwemo klabu ya AS Vita ya Congo.
HARUNA Niyonzima na Obrey Chirwa, wameelezwa kuwa mbioni kupishana milango ya makazi ya klabu zao kwa wawili hao kila mmoja kuhamia upande wa mwenzake.

Niyonzima kwa sasa amejihakikishia nafasi katika kikosi cha Simba chini ya Kocha Mbelgiji, Patrick Aussems, akikumbukwa kwa kiwango cha hali ya juu kilichochangia timu hiyo kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuichapa AS Vita ya DR Congo mabao 2-1 hivi karibuni.
Lakini taarifa zilizopatikana jijini Dar es Salaam juzi na jana, zinasema kuwa kiungo huyo fundi, anatajwa kuelekea kutua Azam ili kutoa nafasi kwa straika wa timu hiyo yenye maskani yake Chamazi, Chirwa, kuhamishia makali yake Msimbazi msimu ujao.
Niyonzima na Chirwa wote mikataba yao inafikia ukingoni mwishoni mwa msimu huu, huku wachezaji hao wakiendelea kuvutana na viongozi wao juu ya kuendelea kuvitumikia vikosi vya timu zao.

Habari za uhakika zilizolifikia BINGWA jijini jana kutoka kwa vigogo wa timu hizo ni kwamba, wachezaji hao huenda wasiongeze mikataba na msimu ujao kuna uwezekano wa Niyonzima kutua Azam na Chirwa kujiunga na Simba.
Kigogo mmoja wa Simba ambaye hakupenda jina lake kuwekwa wazi, alisema licha ya Aussems kupendekeza kuongezwa mkataba wa Niyonzima, lakini bado suala hilo lipo kwa mchezaji huyo ambaye bado hajaweka wazi kuendelea na timu yake hiyo msimu ujao.

Naye kiongozi wa Azam, alisema: “Chirwa tayari ameshaonyesha nia ya kuhitaji kuichezea Simba, kwani hadi sasa tunaendelea na majadiliano, kama ikiwezekana tunaweza kufanya kama ilivyokuwa awali, maana tuliwahi (Azam) kumchukua Abdulhalim Humud na kuwapa (Simba) marehemu Patrick Mafisango.”

BINGWA lilimtafuta Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam, Abdulkarim Amin `Popat`, kuzungumzia suala hilo ambapo alisema kwa sasa wanaendelea na majadiliano na Chirwa ili kuongeza mkataba mwingine baada ya ule wa awali kuelekea ukingoni.
“Ni kweli tunaendelea na mipango yetu ya kuwaongezea mikataba wale ambao ile ya awali inamalizika, tayari tumeshamalizana na Ngoma (Donald) pamoja na Bruce Kangwa, sasa hivi tunazungumza na Chirwa,” alisema.
Kwa upande wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori, alisema wanafahamu juu ya baadhi ya wachezaji wao kumaliza mikataba na sasa wameanza kuifanyia kazi kwa kuzungumza na mawakala wao.

 “Tumepokea ripoti, kocha anataka wale wachezaji ambao mikataba inaelekea ukingoni, waongezewe mingine, tayari wengine tumeshaanza nao mazungumzo na muda wowote tutamalizana nao,” alisema.
Juu ya Niyonzima, alisema japo wengi wanadhani ataondoka, lakini hadhani kama itakuwa hivyo kwani wameshaanza naye mazungumzo huku wakiamini ataendelea kuwapo Msimbazi msimu ujao kwani kocha anamwamini.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list