Nahodha wa kikosi cha Yanga Ibrahim Ajib hajasafiri na timu hiyo kuelekea mkoani Mwanza ambapo keshokutwa Jumamosi itashuka katika uwanja wa CCM Kirumba kuikabili Alliance Fc kwenye mchezo wa robo fainali, kombe la FA
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema Ajib hakujumuishwa katika kikosi kwa kuwa bado hajawa 'fit' tangu apone majeraha ya misuli
Zahera amesema Ajib anahitaji muda zaidi wa kufanya mazoezi ili aweze kuwa tayari kurejea dimbani
Akizungumzia mchezo huo, Zahera amesema wamejiandaa kikamilifu kuikabili Alliance Fc ambayo inaonekana kupania zaidi mchezo huo
"Tunaufahamu ubora wa Alliance Fc na hata udhaifu wao pia tunaujua, hatuna wasiwasi kuelekea mchezo huo," amesema Zahera
Mcongoman huyo aliyerejea usiku wa kuamkia jana na kuungana moja kwa moja na kikosi cha Yanga, amesema atatumia siku ya leo na kesho kufanya maandalizi ya mwisho tayari kwa mchezo huo utakaopigwa Jumamosi March 30 katika dimba la CCM Kirumba
No comments:
Post a Comment