Mahakama ya jumuiya ya Afrika Mashariki imetoa hukumu ya kesi ya kupinga ukandamizaji wa uhuru wa vyombo vya habari chini iliyokuwa imewasilishwa na Baraza la habari Tanzania (MCT) na kituo cha sheria na a haki za binadamu pamoja na Mtandao wa utetezi wa haki za binadamu.
Katika hukumu hiyo ya kesi namba 2 ya mwaka 2017 iliyosomwa na Jaji wa mahakama hiyo Charles Nyachae mahakama hiyo imeitaka serikali ya Tanzania kurekebisha baadhi ya vifungu vya sheria kwani vimeonekana kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari
Akizungumza baada ya hukumu hiyo kutolewa Katibu Mtendaji wa Baraza la habari Tanzania Bw Kajubi Mukajanga amesema haki imetendeka na ameendelea kuwataka wadau wa vyombo vya habari wakiwemo waandishi , wahariri kuendelea kutekeleza wajibu wao na akasisitiza umhimu wa kufuata sheria. Mwaka 2016 Bunge lilipitisha sheria ya huduma za habari,sheria ambayo wadau wa habari na wanaharakati waliilalamikia na kuipinga kwa kile kilichodaiwa kukandamiza uhuru wa habari.

No comments:
Post a Comment