We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Saturday, March 23, 2019

WAZAZI ACHENI KUWACHAGULIA WATOTO WACHUMBA

Wazazi kwa ujumla, watoto tulionao sasa ni kizazi kingine kabisa si kama chetu ambapo kijana alipotaka kuoa ilikuwa lazima mzazi amkubali binti husika.
Mada hii nimeipata kwa msomaji mmoja anayeishi mkoani aliyenipigia simu na kuniambia kuwa mama yake mzazi ni kikwazo kikubwa kwani amekuwa akimchagulia mke wa kuoa, mbaya zaidi ameshampelekea kila aina ya mwanamke lakini bado hakutaka.
“Mama alinipa sharti gumu na kuniambia kuwa kama itafikia wakati wa mimi kuoa nihakikishe nampelekea mwanamke wa kumuoa kwanza ili amtathmini.

“Kwa kuanza nilimpelekea mwanamke ‘Kuku wa kienyeji’ hakumkubali nikaamua kumpelekea wa Kizungu lakini wapi, nilipoona wote hawataki nikaingia kwenye uhusiano na mwanamke wa Kiarabu ambaye nilimpelekea nikahisi atamkubali lakini naye alimkataa.
“Baada ya wote kuwa shida, kwa kuwa nilikuwa nafanya kazi kwenye kampuni ya Wahindi, nilikuwa na ukaribu na mtoto wa bosi nikampeleka kwa nia ya kumpima, pia akamkataa.
“Tabia ya mama kuwakataa wanawake niliokuwa nahitaji kuingia nao kwenye uhusiano ilinichanganya sana hivyo nikaamua kuoa kwa nguvu mwanamke niliyemtaka.

“Tangu hapo mama amekuwa akinifanyia visa kila kukicha anakuja nyumbani kwangu na kuchukua madaraka ya mke wangu, kama kunifulia hata nguo ambazo hazistahili, kiukweli namshangaa sana na sina la kufanya,” alisema kijana huyo.
Wasomaji wangu, bila shaka mmeelewa kitu, akina mama wamekuwa vikwazo watoto wao kuoa kisa kuwachagulia wachumba, hivi kwa nini usimpe uhuru mtoto achague yule anayeona anamfaa?
Kumbuka kumchagulia mwanao mke ndiyo mwanzo wa kumyumbisha, mwanaume anapochagua mke wa kumuoa huwa anajua vigezo anavyotaka hasa vya maendeleo.

Unakuta mwanaume anasoma na binti ambaye wameshakubaliana na amependa kuingia naye kwenye safari ya maisha kwa sababu fulani, sasa wewe unapomtafutia mwanamke mwingine kisha wazazi wake mnafahamiana huoni kama unatafuta mambo mengine makubwa ambayo yataufanya uhusiano wako na wa mwanao kuwa mbaya?

Wazazi wenye tabia hiyo nawasihi mbadilike kwani ulimwengu wa sasa ni wa utandawazi, mnachotakiwa kufanya ni kukaa chini na watoto wenu kuzungumza nao taratibu na kuwapa sababu zinazoeleweka si kukurupuka tu na kumzuia mtu ile roho imependa, unaweza kujikuta unampoteza bure.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list