Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Bashiru Ally amewataka wanachama wa CCM kutobeza na badala yake kuheshimu alama za vyama vyote vya siasa nchini kwa sababu vimesajiliwa kisheria.
Dk Bashiru amesema hayo leo Jumamosi Machi 23, 2019, wakati akizindua mkakati wa kukomaza demokrasia kwenye mashina ulioandaliwa na CCM mkoa wa Dodoma.
“Sisi wanachama wa Chama cha Mapinduzi tunao wajibu wa kulinda Uhuru wa Vyama vingine vilivyosajiliwa kisheria, Kama sisi tunafurahi na kuimba Nyimbo Zetu acheni na wao wafurahi na kuimba Nyimbo Zao, Kama sisi tunapendeza na nguo zetu acheni na wao wapendeze na nguo zao, tunaowajibu wa kuisimamia serikali katika kulinda uhuru wa vyama vya siasa vilivyosajiliwa kisheria hasa katika kipindi hiki ambapo tuaelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu” amesema dkt Bashiru

No comments:
Post a Comment