Baraza la Wadhamini la klabu ya Yanga kupitia kwa Mwenyekiti Mh George Mkuchika limetangaza tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo kuwa ni April 28 2019
Akitangaza mapendekezo hayo, Mh Mkuchika amesema uchaguzi huo utasimamiwa na Wanayanga wenyewe, Shirikisho la soka nchini (TFF) litatuma waangalizi tu
Aidha wakati wa kipindi hiki cha mpito, kutakuwa na Kamati Maalum ya kuisimamia timu huku Kamati nyingine ikiundwa kwa ajili ya kusimamia mchakato wa uchaguzi
No comments:
Post a Comment