Serikali kukatia rufaa uamuzi wa Mahakama ya Afrika Mashariki kuhusu vifungu vya Sheria ya Huduma za Habari ambapo imetakiwa kuhakikisha vinaendana na Mkataba wa Jumuiya Ya Afrika Mashariki
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema Sheria ilitungwa na Serikali ili kuendana na matakwa ya UNESCO kwamba vyombo vya habari vijiongoze vyenyewe.
Amesema kilichofanywa na Mahakama ni kuchomoachomoa baadhi ya vitu na kufanya sheria isikae vizuri, jambo ambalo hawawezi kukubaliana nalo
Amesema Mahakama imetaka kubadilishwa kwa vipengele vinavyozungumzia usalama wa Taifa jambo ambalo haliwezekani kwani hata mikataba ya kimataifa inataka kuwe na uhuru lakini maslahi na usalama wa taifa viwe mbele
Msemaji wa Serikali ameongeza kuwa Mahakama imesema vifungu vya 19, 20 na 21 vinakiuka mkataba wa Afrika Mashariki lakini moja vifungu hivyo kinataka Idara ya Habari kuwatambua na kutoa vitambulisho kwa wanahabari vitakavyowatambulisha katika sehemu za kazi kama serikalini na mashirika binafsi.
Anaeleza kuwa haelewi ni kwanini Mahakama inaweza kuona ubaya katika suala hilo ilhali waandishi wanateseka kwa kukosa utambulisho hivyo anaamini hiyo itakuwa “point” kubwa katika rufaa ya Serikali.

No comments:
Post a Comment