We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Thursday, March 28, 2019

Tundu Lissu Ampa Siku 14 Spika wa Bunge Amlipe Mshahara, Vinginevyo Ataenda Mahakamani

Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA)  Tundu Lissu amesema ameandika  barua  kupitia kwa mawakili wake kwa uongozi wa Bunge, akishinikiza kulipwa mshahara na stahiki zake ndani ya siku 14, lasivyo ataushtaki mahakamani uongozi wa Bunge .

Lissu amesema aliwaagiza mawakili wake kuwasiliana na uongozi wa Bunge ili kufahamu ni lini wataanza kumpatia tena mshahara wake na stahiki za kibunge.

“Mawakili wangu wamemwandikia barua Katibu wa Bunge, Kagaigai ya kumtaka kulipa mshahara na posho zangu za kibunge za tangu Januari mwaka huu. pia walimpa siku 14 kutekeleza madai, vinginevyo tutafungua madai Mahakama Kuu”, amesema Lissu na kuongeza;l



“Bunge halina mamlaka yoyote ya kisheria kuzuia au kukata au kupunguza mshahara wa mbunge na posho zinazotokana na ubunge, isipokuwa tu kama mbunge husika amesimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge kwa azimio la Bunge kutokana na kukiuka maadili ya kibunge.”

“Na hilo haliwezi kufanyika bila kwanza Spika wa Bunge kuielekeza Kamati ya Maadili na Mamlaka ya Bunge kushughulikia suala hilo kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge.”

Machi 14, 2019 Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu aliibua madai ya kutoingizwa  mshahara wake na Mhimili wa Bunge madai ambayo Spika wa Bunge, Job Ndugai alijibu kuwa alipaswa kuuliza uongozi wa Bunge juu ya mshahara wake.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list