Tetesi za Usajili : Wachezaji wawili wanatoka Simba kwenda Yanga
Ligi kuu soka ya Tanzania bara kwa sasa ipo kwenye duru la lala salama huku baadhi ya timuzikiwa zimesaliwa na mechi 10 tu kabla ya ligi kuu kufika tamati.
Baada ya ya Ligi kuisha basi ni wazi kitu kikubwa kitakachokuwa kinafuata itakuwa ni dirisha kubwa la usajili ambapo timu mbalimbali zitaingia kwenye dirisha hilo.
Kuelekea huko Kuna tetesi za chini kwa chini kuwa Yanga inaweza ikawasajili wachezaji haruna Niyonzima na Said Hamis Ndemla ambao kwasasa ni wachezaji wa Simba.
Naye Afisa habari wa Yanga Dismas Ten amekuwa akipost picha za mchezaji wa Simba Said Ndemla na jana akapost picha ya Ndemla akiwa na Haruna Niyonzima huku akionyesha alama ya kurejea (Back Emoji), Wengi wakitafsiri kurejea kwa Niyonzima Yanga na Ndemla ambaye toka mwanzo wa Wiki hii amekuwa akimpost na kuandika ujumbe kana kwamba anatua Jangwani.
No comments:
Post a Comment