Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli ameungana na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na maelfu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuuaga mwili wa aliyekuwa mwasisi na mkurugezi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba aliyefariki dunia Februari 26, mwaka huu nchini Afrika Kusini alikokuwa kipatiwa matibabu.
Rais Magufuli leo Machi 2, 2019 ametoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu Ruge Mutahaba katika viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam pamoja na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mawaziri, Wabunge na viongozi mbalimbali wa vyama na siasa.
No comments:
Post a Comment