Wakati msimu ukielekea ukingoni, tetesi za usajili zinazomuhusu kiungo wa Yanga, nahodha Ibrahim Ajib zimezidi kupamba moto ambapo inadaiwa fundi huyo wa mpira tayari amesaini mkataba wa awali kurejea katika klabu yake ya zamani Simba
Mkataba wa Ajib unamalizika mwishoni mwa msimu hivyo kwa muda uliobaki anaruhusiwa kufanya mazungumzo na timu yoyote ikiwemo kusaini mkataba wa awali
Ajib ni miongoni mwa wachezaji wa Yanga ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu
Kaka yake Athumani Ajib, ambaye ndiye wakala wake, alisitisha mazungumzo ya kuongeza mkataba wa mteja wake hadi mwishoni mwa msimu
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera aliuagiza uongozi wa timu hiyo umalizane mapema na wachezaji ambao anawahitaji kwa ajili ya msimu ujao, Ajib akiwa mmoja wao
Yanga imepania kufanya usajili wa nguvu mwishoni mwa msimu ambapo Bilioni 2 za Kitanzania zitatumika kusajili pamoja na kulipa mishahara ya wachezaji
Hata hivyo huenda ikakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa wapinzani wao Simba ambao wamekuwa na kawaida ya kuwahi kuwasajili wachezaji wanaowaniwa na Yanga licha ya kuwa wachezaji wengi waliowasajili kwa mtindo huo wamekosa nafasi ya kucheza
Hata hivyo kocha Zahera amesema ameshakamilisha mazungumzo na wachezaji saba wa kigeni, kinachosubiriwa ni fedha za usajili
Zahera ametaka fedha hizo zipatikane kabla ya mwezi wa nne kumalizika ili Yanga ikamilishe masuala yake ya usajili mapema kwani amesema kusubiri mpaka mwishoni mwa msimu kutaongeza gharama za michakato ya usajili

No comments:
Post a Comment