Mabosi wa timu ya Simba SC wamemnunulia gari mpya Kocha Mbelgiji, Patrick Aussems katika kuhakikisha kikosi cha Simba kinafanya vizuri kwa kuwekwa hamasa ya nguvu.
Gari hilo ambalo ni aina ya Toyota Wish, Aussems ameanza kulitumia jana wakati kikosi cha Simba kikijifua kwenye Uwanja wa Bocco Veterani kwa ajili ya mechi zijazo za ligi.
Awali Kocha huyo alikuwa akitumia gari ambayo ilikuwa inatumiwa na Makocha waliopita akiwemo Joseph Omog, Jackson Mayanja na Pierre Lechantre.
Taarifa zinasema Aussems aliomba kubadilishiwa ndiga hiyo ili aweze kutimiza majukumu yake ya kazi vizuri na kwa ufasaha zaidi.
Wakati huo kikosi cha Simba kinaendelea kujiandaa na mechi ya ligi ambapo wikiendi ijayo kitakuwa na mchezo dhidi ya Mbao FC, mechi ikipigwa Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.


No comments:
Post a Comment